Msanii wa muziki wa hip hop, Jay Moe amedai aliyekuwa msambazaji wa albamu za muziki wa bongo ‘Mamu’ hakuwahi kuwanyonya wasanii kama baadhi ya watu wanavyodai.
Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Nisaidie Kushare’ amedai kuwa msambazaji huyo alizidiwa ujanja na baadhi ya maharamia wa kazi ya sanaa.
“Unajua wakati ‘Mamu’ analalamikiwa kwamba anawaibia wasanii, yeye pia alikuwa akilalamika kuwa anaibiwa ndiyo maana hata nakala zetu tulizokuwa tunaziuza yeye alikuwa anataka ‘stamp’ za kila msanii ili aweze kupambana na wale maharamia na hata mtaani tulikuwa tunazikagua tukikutana na wamachinga kwa hiyo siyo kweli kama alikuwa anatunyonya maana wapo wasanii wengi waliowahi kufaidika na uwepo wake kama kina Ferooz, Prof Jay, Juma Nature na wengine,” alisema Jay Moe.
Pamoja na hayo Jay Moe amefunguka na kuongeza kuwa “Kelele za wasanii kuhisi kwamba wanaibiwa na Muhindi huyo ndio chanzo cha kuachana na uuzaji wa albamu lakini pia muhindi huyo kushindwa kuendana na utandawazi ndicho kilichomfelisha katika suala la kuendelea kuuza albamu,” Jay Moe
No comments:
Post a Comment