Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli,amesema anaendelea kula sahani moja na wapiga dili na wahujumi uchumi hadi watakapokoma ili kuondoa umaskini uliopo nchini.
Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uwanja wa Bwawani Kibaha, wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku tatu.
“Wataula wachuya kwa uvivu wa kuchagua,nitawabana wezi wote ili hali tuweze kuondokana na usindikizaji wakati sie ni matajiri, wezi ni wezi tuu,hata kama kiongozi mla dili ni mwizi tuu,tumelaliwa vyakutosha ,tumechezewa sana hivyo sasa nipeni ruhusa nilale nao mbele ili tuweze kunufaika na rasilimali zetu,”alisema rais Magufuli.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Kibaha,Silvestry Koka, alisema wananchi wa Kibaha wanamuunga mkono juhudi za rais Magufuli anazoendelea nazo na hatua ya kuinua uchumi kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
No comments:
Post a Comment