Pamoja na Abdi Banda kueleza anakwenda nchini Afrika Kusini kucheza soka la kulipwa, taarifa za uhakika kutoka ndani ya Simba, zinaeleza tayari wachezaji hao walishazungumza na uongozi wa Simba.
Imeelezwa walikutana na kuzungumza kuhusiana na suala lake la usajili.
"Banda alizungumza na uongozi kuhusiana na usajili wake na walikubaliana vizuri kabisa.
"Kilichokuwa kimebaki ni suala la usajili tu. Sasa inashangaza kama utasikia kuwa ameamua kuondoka," kilieleza chanzo cha uhakika.
Juzi, Banda aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram, akiwaaga mashabiki wa Simba baada ya kuwa amecheza mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Mbao FC na Simba kubeba ubingwa.
No comments:
Post a Comment