Msanii wa muziki wa hip hop, Nyandu Tozi, kutoka B.O.B Micharazo amefunguka kwa kuwaponda kundi la Weusi kuwa hawana mafanikio yoyote waliyoyapata katika maisha sababu bado wanaishi katika nyumba za kupanga.
Rapa huyo amesema hayo baada ya kuulizwa swali juu ya ukimya wao katika muziki pamoja na mafanikio waliyoweza kuyapata kama kundi ukilinganisha na Weusi kutoka jiji la Arusha.
“Ukiniambia Weusi wana maendeleo kuliko B.O.B unanishangaza wakati wao wamepanga, B.O.B kila mtu anaishi katika ‘empire’ zao,” Nyandu alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV “B.O.B Micharazo ni ukoo kwa hivyo unavyoona B.O.B wapo kimya katika muziki utakuta labda sasa hivi wapo ‘busy’ mambo mengine kwa sababu watu wana majukumu yao binafsi siyo kwamba tutegemee muziki tu ‘a hundred percent no’ lazima ujishughulishe na uwe na biashara au uwe na maduka ni vitu ambavyo ‘movement’ vijana wengi wasasa wameamka hakuna kijana ambaye amekaa tu ategemee atoe nyimbo i-hit afanye ‘show” Nyandu alifunguka.
Pamoja na hayo, Nyandu amesema kundi lao la B.O.B Micharazo haliwezi kufa kutokana na ukimya wao wa muda mrefu katika ‘game’.
No comments:
Post a Comment