BARAKA ANA CHUKI NA MIMI ASEMA BEN POL - JONGOTZMEDIA.COM

Latest

efm

">">WHATSAPP NUMBER 0757357341

Pages

Friday, 9 June 2017

BARAKA ANA CHUKI NA MIMI ASEMA BEN POL

Baada ya Barakah The Prince kuuponda wimbo mpya wa Ben Pol ‘Tatu’ kwa kudai ni mbaya, Ben Pol amefunguka kwa kudai kuwa muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Acha Niende’ ana chuki binafsi juu yake.
Ben amedai maoni ya Barakah The Prince yanaweza kuwa ni mazuri ya kuboresha na kujenga lakini anaona msuguano katika maoni hayo kutokana na mahusiano yao yalivyo hivi sasa .


“Hii source ya kutuchukia mimi na Jux ni kwasababu tulimpunguza kwenye umoja ambao tulikuwa tumeuanzisha wa kufanya show/tour hatukuwahi kusema hatukutaka kumuaibisha kwenye media na ilikuwa ni lazima tumpunguze kwasababu ya kukosa nidhamu,” alisema Ben Pol.
Aliongeza, “Mnapokuwa mnafanya kazi na mtu halafu mwengine ndio anakuwa Super Star halafu ni mdogo wenu, mnaenda kwenye Interview hatokei, mnahitaji kwenda kufanya sound check yeye kajifungia hotelini na msichana yani vitu hovyo hovyo ikabidi tumpunguze kwasababu inaonekana focus yake ipo chini halafu ukimwambia haelewi. Kuanzia hapo ndio chuki ilipoanza sasa akitoa mawazo unaya-dout kidogo mawazo yake mimi napenda sana kupokea ushauri lakini inakuaje unapewa maoni na mtu ambae anakinyongo sasa hata mara ya mwisho nimemcheki unajua jibu lake ‘Shida yako nini’? ni message ya kawaida tu ya kishkaji halafu kesho unamsikia kwenye Radio eti anasema ‘mimi Ben Pol rafiki yangu sana nampenda sana’ ni unafki, lakini kwa yote mimi nampenda sana Barakah ni mdogo wangu”
Ben Pol, Barakah The Prince pamoja na Jux waliungana kwa pamoja na kufanya show ya pamoja iitwayo, LML ambayo ilifanyika kwa mara ya kwanza siku ya Valentine’s.
Pia katika mahojiano mbalimbali ambayo walikuwa walifanya walieleza kuwa shows za namna hiyo wangeendelea kuzifanya katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment