TUNAOMBA RADHI --SAUDI ARABIA SOKA - JONGOTZMEDIA.COM

Latest

efm

">">WHATSAPP NUMBER 0757357341

Pages

Friday, 9 June 2017

TUNAOMBA RADHI --SAUDI ARABIA SOKA

Shirikisho la Soka la Saudi Arabia (SAFF), limeomba radhi kwa kusahau kuwa kimya kwa dakika kadhaa kama ishara ya kuomboleza shambulio la kigaidi lililotokea jijini London kabla ya mechi ya timu yao ya taifa dhidi ya Australia.
Wachezaji wa timu ya taifa ya Australia wakiwa wametulia kwa muda kuomboleza shambulio la London
Taarifa iliyotolewa na (SAFF) ilisema, “Tunaomba radhi kwa kosa tulilotenda kutokana na wawakilishi wetu kusahau kukaa kimya kwa dakika kadhaa kuomboleza shambulio la London.”
Shirikisho la Soka la Saudi Arabia (SAFF)
Shambulio hilo lilitokea Juni 3 na kuua watu saba, huku wengine kadhaa wakijeruhiwa. Hilo ni tukio la pili wakati lingine lilitokea mwezi Mei.
Wachezaji wa timu ya taifa ya Australia wakishangilia baada ya kufunga bao
Shirikisho hilo lilisema kwamba linapinga vikali vitendo vyote vya kigaidi na linaungana na wanafamilia wote wa walioathirika kwa namna moja ama nyingine nyingine.
Katika mchezo huo  Saudi Arabia walikubali kipigo cha magoli 3-2 ikiwa ni mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia hapo mwakani.

No comments:

Post a Comment