HATIMAYE YANGA WAMRUHUSU NIYONZIMA ASAINI SIMBA BILA PRESHA YOYOTE - JONGOTZMEDIA.COM

Latest

efm

">">WHATSAPP NUMBER 0757357341

Pages

Wednesday, 21 June 2017

HATIMAYE YANGA WAMRUHUSU NIYONZIMA ASAINI SIMBA BILA PRESHA YOYOTE

Baada ya vuta nikuvute ya muda mrefu, hatimaye Klabu ya Yanga imethibitisha kuwa imeshindwa kumsainisha mkataba mpya kiungo wake, Haruna Niyonzima na sasa anaweza kusaini klabu nyingine yoyote.
Simba ndiyo ambayo ilikuwa ikimuwania mchezaji huyo lakini akaomba muda amalizane na Yanga kwa kuwa ni klabu aliyoitumikia kwa miaka sita, alifanya hivyo ili kusikiliza ofa ya Yanga kisha kama wakishindwana basi atasaini Simba.
Kupitia taarifa rasmi ya klabu, Yanga imeafafanua jinsi ilivyokuwa kwa kuandika haya:

TAARIFA KWA UMMA
Klabu ya Yanga kupitia kwa Katibu Mkuu Boniface Mkwasa inapenda kuwajulisha wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga juu ya mchezaji raia wa Rwanda, Haruna Niyonzima ambaye amekuwa mchezaji wetu kwa misimu 6 mfululizo katika kiwango cha juu.
Hata hivyo, Haruna Niyonzima bado ana mkataba mpaka mwezi Julai na Yanga SC, lakini hatutaweza kuendelea kuwa naye kwa msimu ujao kwani hatukuweza kufikia mwafaka katika mazungumzo yetu na yeye licha ya timu yetu kuwa na nia za kuendelea nae kwa misimu miwili ijayo.
Klabu inamtakia kila la kheri katika maisha yake na soka kwa jumla.

Imetolewa na Idara ya Habari na Maelezo
Young Africans Sports club
21-06-2017

No comments:

Post a Comment