Baada ya headlines za muda mrefu kuhusiana na hatma ya kiungo wa kimataifa wa Rwanda anayeichezea Dar es Salaam Young Africans Haruna Niyonzima kuhusishwa kuhama Yanga na kujiunga na Simba baada ya mkataba wake kumalizika.
Leo June 21 2017 Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa ametangaza na kuweka wazi kuwa Haruna Niyonzima ambaye mkataba wake na Yanga unamalizika July, wameshindwa kufikia makubaliano ya kumuongezea mkataba mpya.
Hivyo ni rasmi sasa baada ya Haruna Niyonzima kuitumikia Yanga kwa misimu sita mfululizo, atakuwa nje ya Yanga kuanzia msimu ujao wa 2017/18, bado haijajulikana rasmi Niyonzima atajiunga na timu gani lakini kwa tetesi zinazoenea ni kuwa Niyonzima atajiunga na Simba.
chanzo millardiayo.com
chanzo millardiayo.com
No comments:
Post a Comment