Download app yangu kupitia chrome http://www.appsgeyser.com/5104826?
Baada ya jarida la Forbes kutoa taarifa kuhusu utajiri wa klabu ya Manchester United ni wazi kwamba kwa sasa wanataka kufanya manunuzi makubwa na kuwaonesha watu nguvu ya pesa waliyonayo haswa katika kipindi hiki ambacho wamekuwa hawana matokeo mazuri ndani ya uwanja.
Baada ya jarida la Forbes kutoa taarifa kuhusu utajiri wa klabu ya Manchester United ni wazi kwamba kwa sasa wanataka kufanya manunuzi makubwa na kuwaonesha watu nguvu ya pesa waliyonayo haswa katika kipindi hiki ambacho wamekuwa hawana matokeo mazuri ndani ya uwanja.
Jose Mourinho anaonekana ni mtu sahihi kurudisha heshima ya United ambayo ilipotea tangu kocha Sir Alex Ferguson alipoamua kustaafu soka, msimu huu pamoja na kumaliza ligi wakiwa nafasi ya sita lakini wamepata ticket ya kucheza Champions League msimu ujao baada ya kuchukua ubingwa wa Europa.
Tayari Mourinho yuko katika mawindo ya kutafuta wachezaji wakubwa ili kuleta upinzani mkubwa katika msimu ujao wa ligi, kati ya wachezaji ambao United wanatajwa kuwataka kwa nguvu zote ni nyota wawili wa Real Madrid Alvaro Morata na James Rodriguez na inaonekana Mourinho anataka kuwachukua kwa pamoja.
Alvaro Morata jioni ya Jumatano aliingia kama sub na kuikoa Hisapania baada ya kuisawazishia bao katika mchezo dhidi ya Colombia ulioisha kwa sare ya bao mbili kwa mbili na baada ya mchezo huo Morata aliulizwa kuhusu James Rodriguez na ndipo jibu lake limewafanya mashabiki wa United roho kuwadunda na kuhisi kwamba wametajwa wao.
Morata alisema “Rodriguez ni mchezaji mzuri sana na nina uhakika mwakani pia nitakuwa naye timu moja” iko wazi kwamba Rodriguez anaondoka Real Madrid na jibu la Morata linaonesha pengine mahali ambapo Rodriguez anaenda ndipo ambapo Alvro Morata pia anakwenda.
Tayari United wameshatuma ofa ya kwanza kwa Alvaro Morata ambayo Real Madrid wameikataa lakini tetesi za chinichini zinaseam James Rodriguez ameshaanza kuulizia uwepo wa jezi namba 10 katika klabu ya Manchester United,ni suala la muda tu tusubiri tuone nini kitatokea
No comments:
Post a Comment