MZEE KIKWETE NA MZEE MKAPA WAACHE WAPUMZIKE ASEMA RAIS MAGUFULI - JONGOTZMEDIA.COM

Latest

efm

">">WHATSAPP NUMBER 0757357341

Pages

Wednesday, 14 June 2017

MZEE KIKWETE NA MZEE MKAPA WAACHE WAPUMZIKE ASEMA RAIS MAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli amevionya vyombo vya habari vinavyowachafua Marais wastaafu, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete huku akivitaka viwaache wapumzike.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo ,Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Barrick ya nchini Canada, Profesa John Thornton walipokutana kuzungumzia sakata la Makinikia.
“Nimesoma ripoti zote mbili hakuna mahali ambapo Mzee Mkapa na Mzee Kikwete wametajwa, vyombo vya habari viache kuwachafua hawa wazee, wamefanya kazi kubwa ya kulitumikia Taifa letu, viwaache wapumzike,” amesema Rais.

No comments:

Post a Comment