WACHEZAJI SITA NDANI YA KAGERA NA NYOSSO YUPO - JONGOTZMEDIA.COM

Latest

efm

">">WHATSAPP NUMBER 0757357341

Pages

Thursday, 15 June 2017

WACHEZAJI SITA NDANI YA KAGERA NA NYOSSO YUPO


Nyosso anasajiliwa Kagera Sugar baada ya kumaliza adhabu yake ya kufungiwa miaka miwili kufuatia kumtomasa makalio mshambuliaji John Raphael Bocco akiwa Azam FC kabla ya kuhamia Simba wiki hii.
Mshabuliaji wa Simba, Peter Mwalyanzi akimtoka beki wa Mtibwa Sugar, Ally Shomari.
Mbali na Nyosso ambaye alifungiwa akiwa anachezea Mbeya City mwaka juzi, Kagera Sugar pia imemsajili kipa Hussein Kipao kutoka JKT Ruvu iliyoshuka Daraja kutoka Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita.  


Wengine ni beki Japhary Kibaya kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, viungo Peter Samson Mwalyanzi, Ludovic Venance na mshambuliaji Omary Daga maarufu ‘Dagashenko’ wote kutoka Africa Lyon iliyoshuka Daraja pia.Tayari Kagera Sugar imempoteza mshambuliaji wake tegemeo, Mbaraka Yussuf Abeid aliyesaini Azam FC wiki iliyopita, huku pia kiungo Babu Ally Seif akiripotiwa kuwa mbioni kujiunga na Yanga. 

No comments:

Post a Comment