NICK MINAJ AMDISS REMYMA - JONGOTZMEDIA.COM

Latest

efm

">">WHATSAPP NUMBER 0757357341

Pages

Saturday, 10 June 2017

NICK MINAJ AMDISS REMYMA

Acha movie iendelee – Ni moja ya kibwagizo kinachopatikana katika wimbo wa Number One Remix wa Diamond aliomshirikisha Davido. Sasa kama ulijua bifu la Nicki Minaj na Remy Ma limeisha utakuwa umechelewa.
Mafahari hao wawili wamekuwa katika beef ya maneno tangu mwezi Disemba mwaka jana, baada ya Remy kuanza kumchana Nicki katika wimbo wake wa ‘SHETHER’ lakini alijibiwa na mrembo huyo wa Young Money alijibu mapigo kupitia nyimbo mbili alizoziachia mwezi Februari mwaka huu.
Niki amedaiwa kurudi tena na kumchana Remy kwenye wimbo alioshiikishwa na 2 Chainz’s “Realize”, “I’ve been winning eight years consistently, at least respect it,” amerap mrembo huyo. “Papoose wrote that ‘Ether’ record, but I broke Aretha record / See this is chess, not checkers / You cannot check the checkers / Did Nas clear that ‘Ether’ record? / Nah, but I will complete the record.”
Mwezi Machi mwaka huu Remy alipohojiwa kwenye kipindi cha Another Round, alionekana kulimaliza bifu lake na Minaj huku akiwachana waliokuwa wakishangilia vita yao hiyo, je kwa kuchanwa tena kwenye wimbo huo ataendelea kubaki kimya au Nicki ndio kachkoza nyuki?

No comments:

Post a Comment