Msanii wa Bongo Fleva, Ben Pol amesema mahusiano yake yaliyowahi kudumu zaidi ni miezi tisa tu.
Muimbaji huyo ameeleza kuwa sababu inayopelekea hali hiyo ni kwamba watu wanaoingia katika mahusiano na yeye huwa na matarajio makubwa na wanapokuta sivyo wanakimbia.
“Miezi tisa ndio longest relationship kwa sababu unajua yaani nimekutana na watu wa aina tofauti, watu ambao wanaokuwa na expectation kubwa zaidi kuhusu mtu flani, kwa hiyo akiingia kwenye maisha yako anakuwa ana vitu tayari ali-picture kwamba Ben Pol tutakuwa tunakula bata every weekend, tunakula bata milioni, tunaenda huku na kule,” Ben Pol ameiambia Choice FM.
“Kwa hiyo mtu anaingia kwenye maisha yako anakuta si mtu wa hivyo ni staa ndio lakini we don’t go to club mara kwa mara, we don’t do this, we don’t do that, kwa hiyo mtu anakuwa disappointed anatoka kwenye mahusiano ndio hicho nime-experience zaidi kwenye mahusiano yangu yaliyopita,” ameeleza Ben Pol.
No comments:
Post a Comment