Kiungo wa Everton, Morgan Schneiderlin yupo nchini Tanzania akiwa na mkewe kwa ajili ya fungate.
Mchezaji huyo ambaye pia ni kiungo wa timu ya taifa ya Ufaransa, atakuwa mmoja kati ya wachezaji wa Everton ambao watatua nchini Julai 13 kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki dhidi mshindi wa SportPesa Super Cup, Gor Mahia.
Schneiderlin kupitia ukurasa wake wa Instagram amepost picha akiwa mbugani na kuandika “First day of our honey moon ❤ #tanzania #safari 😍😍!”
Schneiderlin alifunga ndoa Juni 12 na mpenzi wake huyo wa muda mrefu aitwaye Camille Sold.
Ujio huo ni mwendelezo wa mastaa wengi wa England kuja Tanzania, wengine waliotua hivi karibuni ni David Beckham na familia yake, Mamadou Sakho, Victor Wanyama na Christian Eriksen.
No comments:
Post a Comment