SportPesa yaipa Simba kiburi: Yatia maguu kwa Okwi - JONGOTZMEDIA.COM

Latest

efm

">">WHATSAPP NUMBER 0757357341

Pages

Tuesday, 20 June 2017

SportPesa yaipa Simba kiburi: Yatia maguu kwa Okwi

Klabu  ya soka ya Simba SC  kwa sasa imezidi kujikita katika kuimarisha kikosi chake kwenye dirisha hili la usajili kwa ku hakikisha inajiweka sawa kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania Bara pamoja na michuano mingine ya kimataifa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zacharia Hanspope (kushoto) akiwa na mshambuliaji Emmanuel Okwi
Kwa udhamini wa kampuni ya kubashiri ya SportPesa  klabu ya Simba inazidi kuwa na nguvu ya usajili msimu huu na hivyo harakati za kumsajili Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emanuel Okwi kuwa jambo jepesi.
Klabu hiyo imeingia mkataba wa zaidi  ya shilingi bilioni 5 huku wakianza kulipwa Shilingi milioni 950 kwa msimu ujao na ongezeko la asilimia 5% kila msimu.
Mpaka sasa Simba imeshafanya usajili wa nahodha wa zamani wa Azam FC, John ‘Adebayor’ Bocco  mchezaji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo kuanzia msimu ujao.
Huku wengine walio sajiliwa ni pamoja na beki kisiki Shomari Salum Kapombe, golikipa, Aishi Salum Manula,  Jamali Mwambeleko (Mbao FC) pamoja na aliyekuwa beki wa African Lyon, Yusuph Mpilipili.

No comments:

Post a Comment