Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinatarajia kukwea pipa leo jioni kwenda Afrika Kusini kwaajili ya michuano ya COSAFA inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 25 mwaka huu.
Kikosi cha Taifa Stars
Akizungumza na vyombo vya habari, kocha mkuu wa timu hiyo, Salum Mayanga amesema kikosi kipotayari kwa michuano hiyo.
“Tumefanya mazoezi kuanzia jumatatu mpaka leo asubuhi, mazoezi ambayo kiujumla naweza kusema tumekwenda vizuri, kwa sababu vijana walifika wote siku ya Jumapili usiku, Jumatatu tukaanza mazoezi mpaka leo asubuhi.
“Afya za wachezaji zipo vizuri, tulipata tatizo kidogo kwa Shabani ambaye yeye alipata matatizo kidogo akiwa mazoezini lakini wachezaji waliosalia wapo katika kiwango kizuri.
“Tunategema kwa mazoezi tuliyoyafanya leo jioni tutafanya safari ya kwenda Afrika Kusini vizuri kwaajili ya mashindano ya COSAFA na kule tutapata nafasi ya kufanya mazoezi siku kama mbili Ijumaa na Jumamosi na tarehe 25 tutacheza mchezo wetu wa kwanza katika mashindano hayo ambayo tumealikwa na tukifanya vizuri tutaendelea tukifanya vibaya tutarejea kwaajili ya CHAN inayotarajiwa kuchezwa Julai 15 mwaka huu” amesema kocha mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga.
No comments:
Post a Comment