Kikosi cha Taifa Stars kipo kambini jijini Dar es Salaam kikijiandaa kwa michuano ijayo ya kuwania Kombe la Castle Cosafa nchini Afrika Kusini, ambapo timu hiyo inatumia viwanja viwili katika mazoezi.
Timu hiyo ambayo ipo chini ya Kocha Salum Shabani Mayanga, imekuwa ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa JK pamoja na ule wa Azam Complex maarufu kwa jina la Uwanja wa Chamazi.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas amesema kuwa ratiba hiyo itaendelea hadi watakaposafiri kuelekea Afrika Kusini kushiriki michuano hiyo:
Aidha, alisema kuwa wachezaji wameshafanyiwa vipimo vya afya kasoro Elius Maguri ambaye hadi jana alikuwa bado hajawasili kambini.
Waliosalia wote wamefanyiwa vipimo vya afya wapo fiti na wameshaanza mazoezi.
Taifa Stars inajiandaa na michuano ya Cosafa inayotarajiwa kuanza Juni 25, mwaka huu. Michuano hiyo, inaandaliwa na Baraza la Mpira wa Miguu la nchi za Kusini mwa Afrika ambako Tanzania - mwanachama wa Cecafa, imepata mwaliko kushiriki.
Tanzania imepangwa kundi A ambako wapinzani wake ni Mauritius, Malawi na Angola wakati Kundi B ni Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe. Timu za Botswana, Zambia na Afrika Kusini kadhalika Namibia, Lesotho na Swaziland zitakuwa na mechi maalumu (play off) ili kuingia robo fainali.
No comments:
Post a Comment