Kipa mpya wa Simba, Aishi Manula amesafiri kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea nchini Afrika Kusini ambapo Simba ipo nchini humo kwa ajili ya kuweka kambi kujiandaa na msimu ujao wa 2017/18.
Manula alibaki jijini Dar kwa kuwa hakuwa amemalizana na klabu yake ya awali ya Azam katika masuala ya kimkataba, lakini jana Julai 31 alitangaza rasmi kuwa amehamia Simba na anatarajiwa kuelekea Afrika Kusini kuungana na wenzake.
Pichani ni wakati Manula alipokuwa akiondoka alfajiri ya leo Jumanne.
No comments:
Post a Comment