Meneja wa Manches, Jose Mourinho amekanusha uvumi kuwa hana mahusiano mazuri na kiungo wa timu hiyo Paul Pogba.
Mourinho ameyasema hayo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari mapema hii leo na kuwataka wanao eneza uvumi huo waache kuwaongopea watu kwakuwa ana mahusiano mazuri na Paul.
Hayo yamekuja baada ya Pogba ambaye anashikilia rekodi ya klabu kwa kusajiliwa kwa pauni milioni 89 kuwa amekuwa akiingia akitokea benchi.
Hata hivyo meneja huyo raia wa Ureno anaamini kuwa Pogba amepoteza uwezo wake uwanjani na atampatia nafasi ya kuanza mchezo endapo atakiri kuwa kiwango chake kimeshuka.
No comments:
Post a Comment