Tangu kuondoka kwa Jose Mourinho kiungo Nemanja Matic amekuwa haaminiwi na kocha wa sasa wa Chelsea Antonio Conte kwani hajapewa muda mrefu wa kucheza uwanjani kama ilivyokuwa mwanzo.
Lakini Mourinho bado anamuhitaji Nemanja Matic ili acheze na Paul Pogba katika kiungo ya Manchester United usajili ambao unasema kila siku katika vyombo vya habari na sasa umekaribia kutimia.
Taarifa zinasema Manchester United na kiungo huyo tayari wameshakubaliana makubaliano binafsi na sasa kinachosubiriwa ni kwa Chelsea kuopokea ofa kutoka kwa United ili waangalie kama ina maslahi kwao.
Mawasiliano kati ya kocha Jose Mourinho na kiungo huyo wa Serbia yanaonekana ni mazuri bado na wako karibu, hii inaweza kuwa nafasi kwa Mourinho mwenyewe kufanya ushawishi wa kumnunua Matic.
Matic anahitajika United kwenda kumpunguzia mzigo Paul Pogba anayeonekana kuelemewa na majukumu mengi katikati ya uwanja huku msaidizi wake bora ambae ni Michael Carrick umri ukielekea ukingoni.
No comments:
Post a Comment