MASKINI NEYMAR! AMWAGANA NA MPENZI WAKE KWA MARA YA TATU - JONGOTZMEDIA.COM

Latest

efm

">">WHATSAPP NUMBER 0757357341

Pages

Saturday, 24 June 2017

MASKINI NEYMAR! AMWAGANA NA MPENZI WAKE KWA MARA YA TATU

Kwa mara ya tatu, staa wa Barcelona, Neymar amemwagana na mpenzi wake, Bruna Marquezine, ikiwa ni miezi michache tangu waliporudisha uhusiano mapema mwaka huu.
Imeelezwa kuwa licha ya kumwagana huko bado wawili hao wameendelea kuwa marafiki.

"Hii itakuwa mara yangu ya mwisho kuzungumzia kuhusu maisha yangu binafsi hasa kuhusu uhusiano, kwa kuwa sipendi kufanya hivyo.

“Ni kweli tumetengana," alisema Neymar ambaye ana umri wa miaka 25.

Akielezea zaidi alisema: "Ulikuwa ni uamuzi wa kukubaliana baina ya pande mbili. Ni mwanamke ninayempenda na ninaamini atakuwa na furaha huko aliko.

Imeelezwa kuwa sababu ya kutengana kwao ni kwa kuwa Neymar alimuomba binti huyo kufunga naye ndoa lakini Marquezine ambaye ana umri wa miaka 21, akakataa.

No comments:

Post a Comment