Licha ya kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuwasili jijini Dar es Salaam kikitokea Afrika Kusini katika michuano ya COSAFA, mshambuliaji
Mbaraka Yusuph amebaki nchini humo kwa matibabu.
Mbaraka ambaye amesajiliwa na Azam FC hivi karibuni akitokea Kagera Sugar alipata majeraha wakati michuano hiyo ikiendelea na kulazimika kukosa michezo mingi, amebaki nchini humo kwa ajili ya matibabu zaidi.
Hayo yametamkwa na Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga ambaye amesema Mbaraka amebaki kwa sababu za kimatibabu lakini zaidi madaktari ndiyo ambao wataendelea zaidi juu ya tatizo lake.
No comments:
Post a Comment