UTANI UNAOSAMBAA MITANDAONI BAADA KUHUSU USAJILI MPYA WA SIMBA - JONGOTZMEDIA.COM

Latest

efm

">">WHATSAPP NUMBER 0757357341

Pages

Friday, 23 June 2017

UTANI UNAOSAMBAA MITANDAONI BAADA KUHUSU USAJILI MPYA WA SIMBA


Baada ya kuwepo kwa taarifa kadhaa wa kadhaa kuhusu usajili wa Klabu ya Simba kuonekana kuwa na nguvu zaidi ya ule wa Yanga na Azam FC, kuna utani umeibuka mitandaoni juu ya maamuzi hayo ya Simba.
Utani huo unaonekana kutawala kwa mashabiki wa Simba ambao wanajinadi kuwa watafanya vizuri msimu ujao wa 2017/18 kutokana na kuonekana kutumia fedha nyingi katika usajili.
Soma hiki kilichoandikwa kuhusu Simba:
Ni Agosti 19, ndani ya Uwanja wa Taifa, SIMBA vs YANGA, Mechi ya Kugombea Ngao ya Jamii. 
Kikosi cha Simba;-
1: Aishi Manula
2: Shomari Kapombe
3: Mohamed Hussein Zimbwe Jr
4: Juuko Mursheed
5: Kotei James
6: Jonas Gerald Mkude (C)
7: Shiza Ramdhan Kichuya
8: Haruna Hakizimana Fadhili Niyonzima
9: John Raphael Bocco "Boko Haramu"
10: Donald Dombo Ngoma
11: Emmanuel Arnold Okwi "Emosting"
ENOCK BWIGANE; "Mwalimu Kashasha, unazungumziaje hii LineUp ya Simba kuelekea mchezo huu wa watani wa jadi..."
MWALIMU KASHASHA; "Ninachoweza Kusema Enock, hii ni kama vile taifa kubwa kama Marekani lipigane vita na tu-nchi tudogo kama Burundi, na Marekani itumie silaha zake za nyuklia, nafikiri unaweza kuona namna gani vita hiyo itakua haiko balance, na kitakachotokea hapo, Marekani italaumiwa na Jumuiya za Kimataifa kwa maangamizi yatakayozaliwa hapo.

“Enock nadhani kubashiri mechi hii ni rahisi mno hata kama refarii wa kati angekua ni Salum Mkemi, bado sioni ni kwa namna gani Yanga watakwepa dhahma hili. Nadhani hii Simba nitaizungumzia zaidi pindi mechi za Kimataifa zitakapoanza, sio mechi zetu hizi ndogondogo. Kwako Enock..."

No comments:

Post a Comment