Beki wa Taifa Stars, Abdi Hassan Banda amefanikiwa kukamilisha mchakato wa kujiunga na Baroka F.C ya Afrika Kusini kwa kusaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga nayo akitokea Simba.
Baada ya kung’ara katika michuano ya Kombe la COSAFA anayofanyika nchini Afrika Kusini akiiwezesha Tanzania kushika nafasi ya tatu, mchezaji huyo wa zamani wa Coastal Unioni ya Tanga nchini Tanzania, sasa anakaribia kwenda kuanza maisha mapya timu hiyo ya Ga-Mphahlele, karibu na Polokwane, Limpopo ambayo inacheza Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
Banda amesema anaondoka Simba aliyoichezea kwa miaka miwili, baada ya kumaliza mkataba wake na hakuwahi kusaini mkataba mpya, hivyo anajiunga na Baroka kama mchezani huru.
Hivyo, Banda atawasili nchini na Taifa Stars kisha baada ya muda atarejea Afrika Kusini kwa ajili ya majukumu yake mapya.
No comments:
Post a Comment