Simba imemsajili beki wa kati wa Mtibwa Sugar na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars,
Salim Mbonde kujiunga na kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao wa 2017/18.
Haji Manara ametupia mtandaoni picha ya Mbonde kwenye ukurasa wake wa instagram ambapo Mbonde anaonekana amevaa jezi ya Simba huku akisaini mkataba.
Alipoulizwa juu ya usajili huo, Kocha wa Mtibwa Sugar, Zubery Katwila alisema hana taarifa lakini akakiri kuona picha mitandaoni.
Mbonde alikuwepo kwenye kikosi cha Taifa Stars ambacho kimeshiriki michuano ya COSAFA 2017 ambacho kimemaliza katika nafasi ya tatu kwenye michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment